Quantcast
Channel: Blogu ya Wananchi
Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

SHULE YA SEKONDARI YA KWANZA TANZANIA KUKARABIWA KWA SH. BIL. 2.46

$
0
0



{Mkuu wa  Mkoa  wa Tanga Chiku Gallawa pichani }

Raisa  Said, Tanga
Mkakati kabambe wa kukarabati Shule ya Sekondari ya Ufundi ya
Tanga ambayo kihisitoria ni shule ya kwanza ya sekondari kujengwa
nchini umezinduliwa rasmi hapa.

Akizundua mkakati huo mjini Tanga Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Luteni
Mstaafu Chiku Gallawa alisema kuwa ukarabati huo una lengo la
kurejesha hadhi ya shule ambayo imesoma watu na viongozi maarufu,
akiwemo Mkuu wa nchi, Jakaya Mrisho Kikwete.

gallawa  alieleza kuwa Kamati maalumu ambayo inashirikisha wakuu wa
zamani wa shule hiyo akiwemo Thadeus Kinala na Mwalimu Mkuu wa sasa
imeundwa kwa ajili ya kusimamia mkakati huo ambao unabaraka za Rais
Kikwete.

Alisema kuwa jumla ya Sh. Bilioni 2.46 zinatakiwa kwa ajili ya
ukarabati huo ambao umepangwa kufanywa kwa awamu.

Awamu ya kwanza ya ukarabati huo, alisema Mkuu huyo ya Mkoa, ambayo
itagharimu Sh. Bilioni 1.059 utahusisha ukarabati wa mbweni, madarasa,
Ofisi ya Utawala, maabara, bwalo la mikutano na chakula, miundombinu
ya maji taka, Nyumba za walimu, kuweka uzio wa shule na uboreshaji wa
sehemu ya kuegesha magari.

ili kutekeleza mkakati huo, Gallawa alisema kuwa Kamati imeandaa
mkutano mkubwa wa wanfunzi wa zamani wa shule hiyo uliopangwa
kufanyika Machi 15 katika bwalo la mkutano la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.

Alisema mkakati mwingine unahusu Chakula cha Hisani ambacho
kimeandaliwa kufanyika mwezi Mei, mwaka huu wakati wa Maonyesho ya
Pili ya Kimataifa ya Tanga.

Shule hiyo ilianzishwa na wajerumani katika majengo ambayo sasa hivi
yanatumiwa na shule ya Old Tanga Sekondari. Shule ilihamishwa katika
majengo mapya yanayotumiwa na shule hiyo hivi sasa mwaka 1966.

Shule hiyo ambayo ilifunguliwa rasmi na Mwalimu Julius Nyerere mwaka
1967 haijapata kufanyiwa ukarabati mkubwa tangu wakati huo.

Aliwataka wanafunzi wote waliosoma shule hiyo kujumuika siku hiyo ya
Machi 15 kwa ajili ya kuweka  mkakati kwa  kuiunga mkoano

Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>