Quantcast
Channel: Blogu ya Wananchi
Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

NAIBU WAZIRI WA CCM AMWAGA VIFAA VYA MICHEZO JIMBONI KWAKE

$
0
0





Raisa  Said,Bumbuli
 Naibu Waziri wa Mawasiliano,Sayansi na Technologia,January
Makamba ametoa vifaa vya michezo katika  jimbo lake vyenye thamani ya
sh.milion 6.5  kwa ajili ya kuwawezesha  vijana kupenda mchezo wa
mpira wa miguu.

Vifaa vimetolewa  katika  shule  kumi  zilizofanya  vizuri  katika
mitihani ya  kidato  cha  pili mwaka jana  pamoja na kata  zote  ni mipira  100,
jezi  pea 10 pamoja  na  kalamu  box 96  ambazo  kila box  lina kalamu
60 .

Makamba  ambae  pia  ni  Mbunge  wa  Jimbo hilo alisema  ameamua
kutoa  msaada huo  kwa  vijana ikiwa ni harakati za kuhamasisha kuinua
sekta ya michezo katika kata zote jimboni mwake

Lengo la kufanya hivyo ni kupata timu ambazo baadae zitakuja kuwa
tishio kwenye medani ya soka mkoani hapa na  Taifa  kwa  ujumla.

"vifaa nilivyotowa ni katika kutekeleza ahadi zangu  nilizozitoa kwa
vijana jimboni humo wakati  wa  uchaguzi  wa mwaka  2010 kuwa nitainua
michezo kwa kwa timu mbalimbali hasa za vijana".Alisema  Makamba

Hata  hivyo Makamba  alitoa wito kwa vilabu vya Mgambo Shooting na
Coastal Union kuweka utaratibu wa kutembelea Jimboni humo ili kuweza
kuangalia wachezaji wenye viwango vya hali ya juu ambao wanapatikana
wilayani kuliko kuchukua wachezaji nje ya mkoa ambao wakati mwingine
wanashindwa kuipa mafanikio timu hizo.

Katibu wa  Mbunge  huyo Hozza  Mandia ambaye ni diwani wa kata ya
Milingano alisema jitihada zinazofanywa na Makamba zinapaswa kuungwa
mkono na wadau mbalimbali wa soka jimboni humo lengo likiwa kuinua
vijana  kimichezo  katiaka kushiriki kwenye michezoya  ndani  na  nje
ya  bumbuli.

  "Kama unavyojua michezo ni ajira ambayo inaweza kuwainua vijana na
ni fursa ya kipekee kwao hivyo tunamshukuru Mh,Naibu Waziri kwa msaada
huu kwani utaweza kuwaondoa vijana kukaa vijiweni ambapo muda mwingi
hufikiria kufanya vitendo viovu badala yake watakuwa wakishiriki
michezo kutokana na kuwa na vifaa vya kuchezea "Alisema Hozza.


           

Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>