Kwa wale tuliokuwa na nia njema na kijana Mnyika tumekuwa tukitumia juhudi sana kumuasa arudi shule akasome lakini ushauri wetu haukuzingatiwa na mhusika.
kufuatia ukaidi wake huo, leo amehadhirika kwa kukosa nafasi na fursa NONO zaidi kisa tu hana hata stashahada (diploma) ukiachilia mbali shahaba ya kwanza.
Kwa ufupi ni kwamba - ndugu Mnyika alikuwa miongoni mwa wajumbe ambao walitakiwa kuwa wenyeviti wa kamati kwenye bunge la katiba kwa mujibu wa maoni ya wajumbe kadhaa.
Lakini kwa bahati mbaya maoni na mapenzi ya wajumbe hao yaliyeyuka ghafla baada ya maamuzi ya kamati ya kanuni kuweka kigezo cha shahada kama hitaji la kuwa mwenyekiti au makamu mwenyekiti kwenye kamati za bunge maalumu la katiba.
Aidha, juhudi kadhaa zilifanywa na wapenzi wa Mnyika kuweza kukipoteza kigezo cha shahada ili kisimzuie Mnyika kuwa mwenyekiti wa kamati mojawapo ya bunge kati ya 12 zitakazo undwa.
Lakini jitihada hizo za wapenzi wa Mnyika hazikuzaa matunda hivyo kugonga mwamba baada ya mhe Simbachawene kusisitiza kuwa hitaji la kuwa na shahada ili uwe mwenyekiti wa kamati ni la kisheria.
Rai yangu: Kama Mnyika kweli ni kichwa kama ambavyo anapambwa na baadhi ya mashabiki wake. Hivi kupata shahada kuna ugumu gani kwake? Si arudi shule ili awe asset kwa taifa kuliko huku kudhalilika kwake kwa kukosa shahada.
"UONGOZI HAUTAKI UJANJA UJANJA"Source:Jamii Forums