Wasanii wa muziki Shilole na Nuhu Mziwanda wameamua kuweka wazi uhusiano wao wa kimapenzi na kudai kuwa wapo tayari kufunga ndoa.
Akizungumza na U heard ya XXL, Clouds FM leo,Shilole na Nuhu wamesema wanapendana sana na wamekuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi kwa zaidi ya miezi mitatu sasa.
“Tunajipanga mambo fulani yakae sawa pamoja na mke wangu kila kitu kitakaa sawa,” alisema Nuhu. “Kweli tunakama miezi miwili ,mitatu tunashukuru Mungu tunapendana kiukweli. Yeye ananipenda na mimi nampenda pia, mimi nipo real kwake na yeye yupo real kwangu kila mtu yupo real kwa mwezake.
Nilikuwa na girlfriend kipindi hicho ila tumeachana, tumegombana siunajua, na nimekaa muda mrefu bila kuwa na girlfriend, yaani mambo yalifanya tukaonana tukapendana hivyo .First time nakumbuka tulikutana studio,alikuja studio Kijitonyama ambapo mimi nilikuwa nafanya kazi natengeneza beat zangu skeleton tukaongea mambo mengi ya kimaisha hatukuwa in deep sana kihivyo, ila tulivyoendelea kujuana tukaona kila mtu akamzoea mwenzie,mimi nikiwa mbali anakasirika na mimi nikiwa mbali nay yeye anakasirika. Kwahiyo end of the day tukawa tunapendana kweli yakawa mapenzi.”
Naye Shilole alidai kuwa ni kweli wanapenda na Nuhu.
“Sijamkana Nuhu,kwanini nimkane kwa sababu gani? Yeye ananipenda na mimi nampenda,” alisema Shilole huku akisema yupo tayari kwa kufunga ndoa na msanii huyo.
“Sijamkana Nuhu,kwanini nimkane kwa sababu gani? Yeye ananipenda na mimi nampenda,” alisema Shilole huku akisema yupo tayari kwa kufunga ndoa na msanii huyo.
CREDIT : BONGO5