Kikosi cha Taifa Stars.
Taifa Stars imefanikiwa kupata sare ya bao 1-1 dhidi ya wenyeji wake Namibia katika mechi ya kirafiki iliyochezwa leo jijini Windhoek.Stars ndiyo ilikuwa ya kwanza kupata bao lililofungwa na kiungo mwenye kipaji wa pembeni wa Azam FC, Hamis Mcha maarufu kama Vialli.
Vialli alifunga bao hilo zikiwa zimebaki dakika tatu tu mpira kwisha, lakini wenyeji wakasawazisha katika dakika za nyongeza. Bao lao lilifungwa katika dakika ya 90+4.