TAMKO KULAANI MATENDO YA KIKUNDI VYA WATU KWENYE MITANDAO YA JAMII
Kumekuwa na muendelezo wa matukio kadhaa kutoka kwa kikundi cha watu kumuhusisha Mh Lowassa na matukio ya uongo na kumzushia vitu vya ajabu kabisa, hususani katika mitandao ya kijamii.
Kumesambazwa picha ya noti ya shilingi Mia tano yenye picha ya Mh Lowassa. Kitendo hicho siyo Utani, bali ni dhihaka na dharau kwa alama za utaifa na mamlaka ya nchi.
Mh Lowassa anaheshimu maoni ya watu na nguvu ya mitandao ya kijamii, lakini anasisitiza umuhimu kwa wananchi kutumia nguvu hiyo ya mawasiliano kwa kujadili maendeleo ya nchi yetu badala ya kuwa watu wa kuzusha mambo yasiyo na tija kwa nchi yetu.
Imetolewa na ofisi ya Mh Lowassa(mb)
Machi 7, 2014