AMINI usiamini lakini ndivyo ilivyo! Utajiri wa Mtangazaji wa Radio Times FM ya jijini Dar, Khadija Shaibu ‘Dida’ umeibua gumzo midomoni mwa watu wakidai kuna walakini juu ya upatikanaji wake.
Toyota Verossa ikiwa imepaki pembeni ya ghorofa analodaiwa kumiliki Dida.
Kwa mujibu wa chanzo makini, Dida ana utajiri mnono lakini anafanya siri ili watu wasiulize alikoupatia kwa sababu si kwa njia halali.NYUMBA MBILI, MOJA YA GHOROFA
Chanzo kiliendelea kudai kwamba mtangazaji huyo wa Kipindi cha Mitikisiko ya Pwani, ana nyumba mbili. Moja ipo Kigamboni na nyingine ipo Goba ambayo ni ya ghorofa moja, zote jijini Dar.
“Ile ghorofa ya Goba ni kiboko. Ina uwanja mkubwa ndani kama wa mpira, kuna maegesho ya magari hata kumi. Kuanzia getini hadi mlango mkubwa kumesakafiwa,” kilisema chanzo.
Magari aina ya Toyota Carina na Verossa yote mali za Dida yakiwa yamepaki.
MAGARI MATANO YA KUTEMBELEAChanzo chetu kikazidi kwenda mbele kwa kudai kuwa mbali na umiliki wa nyumba, pia mwanadada huyo ana magari matano kwa ajili ya kutembelea tu.
“Mbali na nyumba hizo, Dida pia ana magari matano ambayo hubadili anavyotaka kwa ajili ya kutembelea tu kwenye mizunguko yake.
“Ana Toyota Verossa mbili, ana Toyota Noah rangi ya silva na nyeusi. Ana Toyota Vitz. Hivi karibuni ameanza mchakato wa kuingiza nchini gari lingine la sita aina ya Range Rover ‘Vogue’. Hebu fikirieni, Dida huyuhuyu mnayemjua, amepata wapi mali hizo?” kilihoji chanzo.
Khadija Shaibu ‘Dida’.
YADAIWA ANAUZA ‘UNGA’Chanzo kilisonga mbele zaidi kwa kusema kuwa, habari za mitaani ni kwamba mtangazaji huyo anatuhumiwa kuuza madawa ya kulevya ndiyo maana ametajirika ghafla.
“Watu wamekuwa wakimsema kwamba fedha zake zinatokana na biashara ya kuuza unga. Si unajua wauza unga wana pesa sana?” kilisema chanzo hicho.
MADUKA MATATU YA NGUO
Katika tafutafuta, mapaparazi wetu waliwahi kuyanasa maduka matatu ya nguo za kike ambayo yapo Kinondoni, mmiliki wake akiwa ni Dida.
Katika mabango ya matangazo, maduka hayo yanasomeka; Dida Classic.
AMETOKA MBALI
Kabla ya kudaiwa kuwa na utajiri huo, wakati fulani Dida aliwahi kukumbana na misukosuko ya madeni ambapo benki moja maarufu jijini Dar es Salaam ilifilisi samani za sebuleni, nyumbani kwake Kinondoni, Dar baada ya kushindwa kulipa mkopo.
Dida akipozi jirani ya gari aina ya Range Rover Vogue alilopanga kulidondosha Bongo.
DIDA ASAKWABaada ya kuzinyaka habari hizo, mapaparazi wetu walimtafuta Dida ili kueleza ukweli ambapo alikuwa na haya ya kusema:
“Mimi sipendi kuanika vitu nilivyonavyo au ninavyomiliki ila ni kweli nina nyumba mbili, moja Kigamboni na nyingine Goba ya gorofa.
KUHUSU MAGARI
“Magari ninayo matatu na si matano, hilo Vogue mchakato unaendelea, ukikamilika nitaliingiza nchini.
MIRADI YA DUKA
“Kuhusu miradi yangu mingine siwezi kuianika hadharani kwa sababu, kwanza sipendi kabisa mambo hayo,” alisema Dida.
Toyota Noah kama anayomiliki Dida.
NI KWELI ANAUZA UNGA?“Watu wamekuwa wakiongea sana kwamba nauza unga kitu ambacho si kweli, kwanza sijui hata huo unga unafananaje! Ila mimi ninajituma sana kwenye kazi pamoja na kufanya biashara mbalimbali.
“Sitasahau siku ambayo watu walikwenda kutoa taarifa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (Dar) kuwa siku hiyo nasafiri na mzigo wa madawa ya kulevya.
“Nilipofika uwanjani nikawekwa chini ya ulinzi na kupekuliwa. Kama haitoshi nilipelekwa Hospitali ya Temeke (Dar) nikafanyiwa X-ray, hawakuona kitu ndipo nikarudishwa uwanja wa ndege kuendelea na safari
“Mimi nawaacha tu waongee watachoka kwa sababu hawajui wanachokifanya, ila mimi najitambua na kile ninachokifanya,” alisema Dida.
Toyota Vitz kama ya Dida.
Akaendelea: “Nilichokuja kubaini ni kwamba kuna wabaya wangu ndiyo walipeleka taarifa za uongo pale uwanjani. Wote huo wivu tu hakuna lingine.“Kuanzia hapo nikaamua kufanya mambo yangu kimya-kimya, hakuna sababu ya kutangaza kwani wabaya ni wengi, wazuri wachache na si kila anayeku-chekea ni mzuri kwako.