picha kwa hisani ya mitandao ya kijamii.
Mbunge wa jimbo la Iringa mjini Mh.PETER MSIGWA kwa mara nyingine amefikishwa leo katika mahakama kuu ya mkoa , kufuatia tuhuma inayomkabili ya kufanya vurugu katika kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani katika kata ya nduli manispaa ya iringa.
Tukio hilo limetoke tarehe 6 ya mwezi wa pili ambapo SALUM KEITA mjumbe wa kampeni hizo kupitia chama cha mapinduzi alidai kufanyiwa vurugu na mbunge wa jimbo la iringa mjini kwa kumpiga.
Kesi hiyo imesomwa leo katika mahakama ya wilaya ya Iringa mbele ya jaji ALOYCE MASUA na kesi hiyo imeahirishwa na kutajwa kusikilizwa
tarehe 9 ya mwezi wa 4 mwaka huu.