Quantcast
Channel: Blogu ya Wananchi
Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

SSRA YATOA ELIMU KWA WASTAAFU WATARAJIWA

$
0
0

Displaying Tagla 5.jpg

















Ili kuhakikisha kuwa elimu ya hifadhi ya jamii inawafikia wadau wote, Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii -SSRA leo hii imetoa elimu kwa Washiriki 45 kutoka Taasisi mbalimbali na Mashirika ya Kiserikali Mkoani Morogoro. Semina hiyo ambayo iliandaliwa na TAGLA ililenga katika kutoa elimu ya mafunzo juu ya kujiandaa na maisha baada ya kustaafu, ambapo Mamlaka ilipewa fursa ya kuwaelimisha washiriki hao juu ya umuhimu wa Sekta ya HIfadhi ya jamii, na Jinsi Mafao ya Pensheni yalivyo mkombozi wa Wastaafu.Akiwasilisha mada kuhusu majukumu ya Mamlaka, Mkuu wa Mahusiano na Uhamasishaji wa Mamlaka hiyo Bi Sarah Kibonde Msika aliezea kwakina jinsi Mamlaka inavyolinda na kutetea maslai ya wanachama na umuhimu na kujiunga na kuendeleza uanachama wa mifuko ya hifadhi ya jamii.Akijibu maswali yaliyoulizwa na wanasemina na hasa swali kutoka kwa Bwana Kindika wa Weight & Measures Mandela, kuhusu Mifuko ya hifadhi ya Jamii kufanya uwekezaji na maamuzi mbalimbali bila kuhusisha wanachama Mkurugenzi wa Tafiti, Tathimini na Sera Bwana Ansgar Mushi, aliwaeleza wanasemina hao, kuwa uwakilishi wa wanachama katika maamuzi ya mifuko upo kupitia Bodi za Wadhamini za mifuko ya Hifadhi wa jamii ambazo baadhi ya wajumbe wake wa bodi hutoka katika Vyama vya waajiri, vyama vya wafanyakazi , Serikalini,na Mwanasheria Mkuu.

Displaying Tagla 6.jpg
Bwn Ansgar Mushi akijibu maswali ya wanasemima

Displaying Tagla 7.jpg
Wadau wakisikiliza mada inayowasislishwa na SSRA


Displaying Tagla 8.jpg
Wadau wakisikiliza mada inayowasislishwa na SSRA

Displaying Tagla 13.jpg
Bwana Ansgar Mushi akiju swali kuhusu formula za mifuko ya hifadhi ya jamii




Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>