Wakazingumza kwa nyakati na mahali tofauti katika Viwanja vya Bunge mjini Dodoma jana, wananchi hao walielezea kutoridhishwa na hatua hiyo.
Kitendo cha Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba kuahirisha vikao vya chombo hicho mara kwa mara, kimewakera baadhi ya wakazi wa mji wa Dodoma.
Wakazingumza kwa nyakati na mahali tofauti katika Viwanja vya Bunge mjini Dodoma jana, wananchi hao walielezea kutoridhishwa na hatua hiyo.
Walisema kwa vyovyote vile, mchezo huo hauwaridhishi Watanzania, kwa sababu ni matumizi mabaya ya rasilimali za nchi.
“Hivi kweli tunataka kutunga Katiba au watu wanaleta usanii hapa. Kura tu kwamba iwe ya siri au wazi ichukue muda wote huoo,” alishangaa Joseph Jonathan.
Alisema kwa mtazamo wake Bunge hilo lingevunjwa kwanza ili kama kuna maridhiano yafanyike nje na baada ya kufikia mwafaka, wajumbe warudi bungeni kupitisha vifungu.
Amina Ally alisema kinachofanya jambo hilo liendelee kuwa zito ni ubinafsi wa baadhi ya wajumbe wa Bunge hilo na makundi yao.
“Kama siyo ubinafsi jambo hilo lingeshafikiwa mwafaka. Watu wanajali zaidi masilahi yao badala ya masilahi ya Taifa zima. Wanajali zaidi kuona jambo linawanufaisha kwanza wao kuliko wenzao na kwa mtaji huu hatutafika mbali,” alisema.
Charles Jackson alisema haoni mantiki ya Bunge hilo kuendelea kama wajumbe hawataki kuweka kando masilahi yao na kujali masilahi ya taifa.
Alisema mabishano yanayojitokeza katika mijadala ya Bunge hilo kuhusu mambo madogo kama aina ya kura inafaa kupigwa wakati wa kupitisha vifungu, ni matokeo ya ubinafsi.
“Huu ni ubinafsi tu ambao hausaidii kujenga zaidi ya kubomoa. Watu wanapaswa kubadilika na kuwa kitu kimoja badala ya kugawanyika kwa misingi ya itikadi ya vyama na maslahi binafsi,” alinena.