Mwanamuziki Victoria Kimani amezitaja sifa za Mwanaume
anayetaka kumuoa kuwa ni pamoja
na anayependa kujirusha hata baada
ya kufikisha miaka 50 au 60.
Alisema anahitaji pia mwanaume mwenye ratiba
ya maisha inayobadilika siku hadi siku.
''Kuna wanaume mambo yao kila siku maisha yao ni
hayo hayo, siyo wabunifu, lakini kuna ambao
kila siku wanakuja na wazo jipya , na
mkitoka mnaelewana'' Alisema Kimani