Quantcast
Channel: Blogu ya Wananchi
Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

ONA WALICHOKISEMA WAKULIMA WA CHAI BUMBULI

$
0
0
                                                        






 Raisa Said, Bumbuli

SERIKALI imetakiwa kufikia maamuzi ya haraka ya kumtafuta mwekezaji mwingine wa kiwanda cha Chai cha Mponde  kilichopo Halmashauri ya Bumbuli  Wilayani  Lushoto ili kuinusuru chai ya wakulima inayoendelea kuharibikia shambani kwa miezi minane sasa.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti  wakulima hao walisema tangu kiwanda hicho kimefungwa mwaka jana chai yao inaendelea kuharibikia mashambani na kuwafanya kuwa na hali ngumu kimaisha  kutokana  na kukosekana soko la uhakika la zap hilo.

Idrisa Mbega mkulima wa Chai katika halimashauri hiyo alisema wakulima wanachokiomba kwa serikali ni kuwafungulia kiwanda chao ili chai yao isiendelee kuharibika mashambani na kwamba kama serikali haitafanya hivyo watakifungua kiwanda hicho wenyewe kuinusuru chai yao.

Hata hivyo  Mkulima mwingine Alimasi Shemshami  alisema baada ya kufikia maamuzi ya kukifunga kiwanda hicho serikali iliunda tume ambaye baadaye ilipendekeza kuundwa kwa uongozi wa muda katika kiwanda hicho ili kiwezesha shughuli za uzalishaji  kuendelea lakini  jambo  la  kusikitisha  hadi sasa uongozi haujaundwa  huku zao  hilo  likiendelea  kuharibika .

Aidha  Kiwanda  cha Mponde  ambacho kinamilikiwa  kwa ubia  kati ya  Umoja wa Wakulima  wa chai{UTEGA} na Mwekezaji  kilifungwa baada  ya wakulima  hao  kugoma kupeleka  maja ni mabichi  wakituhumu  mwekezaji  huyo  kuwa  anawanyonya  kwa kununua  bei  ndogo  zao hilo, pamoja  na kutokuwalipa kwa  wakati.

Pia jambo lingine  ambalo  kwa muda  mrefu  wakulima  hao wamekuwa wakilalamikia  ni pamoja  na  kuutuhumu  uongozi  wa UTEGA  kuwasehemu ya mwekezaji hivyo kushindwa  kutetea  maslahi  ya wakulima ambao waliwachagua.


"Maamuzi ya kufungwa kwa kiwanda tuliyafanya sisi wakulima na tulifanya hivyo kwa maslahi yetu ,sisi maamuzi yetu hatumtaki mwekezaji pamoja  na  UTEGA ,tunachotaka ni kumpata mwekezaji mwingine huyuhapo tulipofikia naye panatosha,"alisema Shemshami.


Kufuatia  hali hiyo  wakulima wa bumbuli  inawalazimu  kusafirisha  zao hilo  katika   viwanda vidogo vya  Dindira,na Hekulu wilayani korogwe  ambapo nyakati  za mvua  zinaponyesha  usafiri huwa mgumu na pia  uwezo wa viwanda hivyo ni mdogo ikilinganishwa na chai wanayozalisha hivyo kujikuta  wakipata  adha  kubwa.

Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Bumbuli Beatreace  Msomisialisema tangu kiwanda hicho kilivyoacha kufanya kazi halmashauri hiyo imeathirika kiuchumi ikizingatiwa kwamba kiwanda hicho kilikuwa tegemezi ya wakulima wengi wanaolima chai katika eneo hilo.

Hata hivyo amewaomba wakulima kuvuta subra wakati serikali ikiangalia namna ya haraka ya kutatua mgogoro huo ambao umedumu tangu miaka kumi na tatu iliopita kabla ya kufungwa rasmi kwa kiwanda kiwanda hicho mwaka jana.

Kilimo cha chai ndicho kilimo pekee kinachotegemewa na halmashauri ya Bumbuli kiuchumi na mgogoro huo umepelekea kurudisha nyuma maendeleo ya wakulima wa chai katika halmashauri hiyo.

    Mwisho.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>