Quantcast
Channel: Blogu ya Wananchi
Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

OMMY DIMPOZ + VANESSA MDEE WAPATA SHAVU KWA VICTORIA KIMANI SOMA HABARI YAO HAPA LIVE!!

$
0
0
WASANII wawili wa muziki wa kizazi kipya nchini Omary Nyembo 'Ommy Dimpoz' pamoja na Vanessa Mdee wamefanikiwa kumshawishi msanii wa kimataifa Victoria Kimani kutengeneza 'collabo'.

Wasanii hao wamefanikiwa kumshawishi msanii huyo, kutokana na kazi zao wanazozifanya na mashabiki wao wanavyozipokea.

Akizungumza katika moja ya mahojiano aliyoyafanya alipotembelea nchini hapa kwa mualiko maalumu, Kimani alisema kuwa amefikiria kufanya nyimbo na Vanessa Mdee kutokana na umahiri wake pamoja na ubunifu alionao.

Alisema kuwa anahitaji mtu mwenye sifa kama za Vanessa hivyo, kukutana na msanii huyo kumezidi kuimarisha dhamira yake ya kufanya muziki na msanii huo na kuamini kuwa utakuwa ni miongoni mwa muziki utakaofanya vizuri katika soko la muziki nchini.

"Naamini Vanessa ni msanii mzuri, tena anauwezo mkubwa hivyo akifanya kazi na mimi nyimbo hiyo itavunja rekodi mbalimbali na itatikisa katika ngazi za kimataifa na soko la muziki" alisema Kimani.

Alisema kuwa kwa upande wa Ommy Dimpoz pia anahitaji kufanya naye collabo, ambapo itaongoza idadi ya wasanii watanzania kufanya naye nyimbo akiwemo AY .

Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>