- Rasimu ya Katiba imependekeza mawaziri wasiwe wabunge ili wawajibike ipasavyo.
Dodoma. Mjumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, John Chiligati amesema mabadiliko ya Katiba yatakayofuta haki ya mbunge kuwa Waziri, yataongeza uwajibikaji kwa umma.
Chiligati aliwahi kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani (2000-2005), Waziri wa Mambo ya Ndani (2006), Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana (2006-2008 na Waziri wa Ardhi mwaka 2008.
“Mhimili wa Bunge ufanye kazi za Bunge na ule wa Serikali ufanye kazi za Serikali na Mahakama ifanye kazi zake. Siyo mtu mmoja kutumikia mihimili zaidi ya mmoja,” alisema.
Kwa mujibu wa Chiligati, kama mapendekezo hayo yatapitishwa na wajumbe wa Bunge la Katiba ina maana kuwa Mbunge hawezi tena kuwa Waziri, Mkuu wa Mkoa au Mkuu wa Wilaya.
“Sasa hivi tuna wabunge ambao ni wakuu wa mikoa au mkuu wa wilaya na mbunge mwingine ni waziri. Tukipitisha hili kwenye Katiba ni kwamba sasa mbunge atabaki kuwa mbunge wa kuwatumikia wapigakura wake basi,” alisema.
Chiligati alisema ingawa pendekezo hilo linaonekana kuwa ni jipya miongoni mwa Watanzania, mgawanyo huo wa madaraka upo pia katika nchi za Kenya na Rwanda na kwamba umeongeza uwajibikaji kwa umma.
“Unajua unapokuwa waziri halafu unakuwa mbunge jambo likija pale bungeni kwa hali ya kibinadamu, unaona haya kumbana unasema ‘aah, huyu ni mwenzetu’,” alisema Chiligati.
“Lakini akishakuwa huyo mnayembana siyo mbunge mwenzenu, kibano kinakuwa kikali na ni kwa manufaa ya umma. Binafsi sioni kama kuna tatizo japo mazoea nayo yana matatizo yake,” alisema. Chiligati alisema mapendekezo hayo yanaelekeza wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano na mawaziri kukutana kwenye Kamati za Kudumu za Bunge.