Waliosimama Kutoka Kushoto : Salum Mbonde,Dickson Daud,Abdalah Juma, Ally Shomary, Shaban Nditi,Walioinama Kutoka Kushoto : Vicent Barnabas, Said Mkopi,ShabanKisiga,Husein Ramadhan, Paul Ngalema
Kikosi cha Timu ya Yanga Kilichoanza Leo : Kutoka Kushoto Didier Kavumbangu, Haroub Canavaro,Khamis Kiiza,Oscar Joshua,Frank Domayo,Simon Msuva, Juma Abdul,Nizar Khalifan,Mbeleni Juma Kaseja.
Ligi Kuu Tanzania Bara Imendelea Leo Ambapo Katiak uwanja wa Jamuhuri Mkoani Morogoro Kulikuwa na Mchezo Mkali Dhidi ya Wenyeji Mtibwa Sugar ya Manungu Turiani Mkoani Morogogo Dhidi ya Mabingwa Watetezi Yanga ya Dar es Salaam . Katika Mchezo Huo Hadi Dakika 90 za Mchezo Zinamalizika Matokeo Timu Hizo Zmetoka sare ya Bila Kufungana.Mchezo Ulikuwa Mkali na wakukamiana Pamoja na Hali ya Uwanja Kutokuwa nzuri kutoka na Mvua Zianzoendelea Kunyesha Mkoani Hapa.Timu ya Yanga walitengeneza Nafasi Nyingi za Kufunga lakini walishindwa Kuzitumia .Wachezaji Emanuel Okwi na Didie Kavumbangu walipata nafasi za kufunga katika dakika ya 80 na 88 lakini awalishindwa kufunga, Yanga walifanya Mabadiliko katika Dakika ya 65 Alitoka Nizar Khalifan na Kuingia Said Dilunga,Dk78 Alitoka Khamis Kiiza na Kuingia Husein Javu.
Mtibwa Sugar Walipata Pigo katika Dakika ya 70 Ambapo Mshambuliaji Wao Abdalah Juma Alionyeshwa Kadi Nyekundu kwa Kumchezea Rafu mbaya.