Taarifa ambazo zimethibitishwa na tovuti ya Yanga kuhusu kunusurika ajali bus walilokuwa wakisafiria kutoka Morogoro kurudi Dar ambapo ni Bus la timu ya Young Africans lililokuwa limebeba wachezaji pamoja na viongozi wa benchi la ufundi limepata ajali eneo la Mikese Mizani baada ya Mabasi yaliyokuwa yakitanua kuelekea mikoa ya bara kuziba njia na kusababisha kutumbukia kwenye mtaro.
Katika ajali hiyo iliyotokea majira ya saa tatu na nusu asubuhi hakuna mtu yeyote aliyejeruhiwa na kwa sasa timu inaondoka na usafiri wa bus jingine kuelekea jijini Dar es salaam