"Kamati ya PAC imemaliza kikao chake na Wizara ya Ardhi, Fungu 48. Wizara imetekeleza agizo la Kamati la kutoa upya hati za umiliki wa Ardhi ambapo kumbukumbu za ardhi zitaunganishwa na mfumo wa namba za mlipa kodi na vitambulisho vya Taifa. Hati salama zisizogushika (ngumu kugushi). Kamati imeridhia mchakato uendelee ili kuanza kazi hiyo kwa awamu na kwa kuanzia na mkoa wa Dar Es Salaam."