Quantcast
Channel: Blogu ya Wananchi
Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

THE MAJANGAZ & BONGO:- KUMBE UYU SUPER STAR WA BONGO FLEVA ALINASWA NA WIFE WA MTU!!

$
0
0


Mkali wa bongo fleva Abelnego Damian 'Belle 9' Aliwahi kukumbwa na zahma mbaya ya kufumaniwa chumbani na mke wa mtu jambo ambalo lilimalizwa kwa kuminywa chini kwa chini lakini habari hiyo haikubumburuka wala kulipotiwa mahali popote.
Kwa mujibu wa chanzo chetu makini ambacho pia ni msanii mkubwa katika game la muziki (jina lipo kwenye droo zetu) Bele alipata kashfa hiyo mwaka 2010 ambapo siku ya tukio alikuwa chumbani kwake na mwanamke huyo ambaye hakujua kama ni "mali ya mtu"
Aidha "mtonyaji" wetu alizidi kuweka bayana kuwa, bahati nzuri Belle 9 alikuwa anafahamiana vyema na mfumaniaji huyo ambapo alikuwa muungwana kwa kuomba msamaha huku akiipoza ishu hiyo kwa  misimbazi kadhaa "ishu haikuwa ya kitoto . Waliyamaliza chumbani humo humo lakini Belle 9 alivunja kabisa uhusiano wa aina yeyote na mwanamke huyo.
Mdakuzi wetu alipomtafuta Belle 9 kwa njia ya simu , alikiri kukumbwa na jambo hilo huku akisisitiza kulisahau. "Duh! hiyo ni kitambo sana ujue, ila anyway ni kweli lakini halikuwa fumanizi kama unavyosema, wala hakuwa mke wa mtu zaidi ya mapenzi ya kawaida" alisema Belle 9.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>