Quantcast
Channel: Blogu ya Wananchi
Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

REAL MADRID,CHELSEA ZAPETA UEFA..

$
0
0
Mcameroon Samuel Etoo na beki Garry Cahil  wameiwezesha timu yao ya Chelsea kusonga hatua ya robo fainali kwa jumla ya magoli 3-1 katika mashindano ya Uefa,kufuatia magoli waliyofunga dhidi ya timu ya Galatasaray.


Etoo ndiye alikuwa wa kwanza kuwanyanyua mashabiki wa klabu ya Chelsea baada ya kuanza kuandika kalamu ya magoli kwenye 4dk ya mchezo kufuatia mashambulizi yaliyoanzishwa na mchezaji fundi wa klabu hiyo Eden Hazard kabla ya kummegea pande mchezaji wa kibrazil Oscar kabla ya beki tegemeo kwasasa ndani ya kikosi hicho Cahil kuihakikishia timu yake ushindi na kuwaonyesha mlango wa kutokea wapinzani wao Galatasaray katika dakika ya 43.

Real madrid pia imesonga mbele katika hatua ya robo fainali baada ya kuitandika mabao 3-1 timu ya schalke na kufanya jumla ya mabao 9-2.Mchezaji bora wa Dunia mreno Cristiano Ronaldo alitangulia kufunga goli la kuongoza dakika ya 22,kabla ya T Hoogland hajasawazisha kwenye dakika ya 31 matokeo yaliyodumu hadi kipindi cha kwanza kinamalizika.
Kipindi cha pili dakika ya 74,Ronaldo tena alifunga bao la pili kabla ya A Morata ajashindilia maumivu kwa timu hiyo ya bundasiliga dakika ya 76.



Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>