Kocha wa timu ya taifa ya Nigeria Stephen Kesh amedai bado mchezaji wa zamani wa timu Peter Odemwingie hana uhakika wa kuwemo ndani ya kikosi kitakachoshiriki mashindano ya kombe la Dunia nchini Brazil badae mwaka huu.
"bado wanaigeria wajaelewa kuusu hili,lakini kwanini tuchukue mda mrefu kumzungumzia Odemwingie au Ikechukwu Uche wakati wapo weni ndani ya taifa hili...” alisema Stephen Keshi.
Keshi alisema kuwa anafuraha kuona mchezaji huyo akifanya vizuri ndani ya klabu yake kwasasa lakini akasisitiza bado haitoshi kwake kumjumuisha katika kikosi hicho cha Eagles.Pia kocha huyo aliongeza kusema timu ya taifa ya Nigeria si timu ya mchezaji mmoja na hakuna mchezaji anayestahili kujiona ni bora zaidi ya mwingine.