Muigizaji Mainda ameonyesha kukerwa kwake na magezeti ya udaku yanyo mchafua kwa kuandika habari za uongo juu yake. Muigizaji huyo ametoa dukuduku lake kupitia ukurasa wake wa Instagram kwa kupost picha zifuatazo zikiambatana na ujumbe kutoka kwake kwenda kwa wahusika.
Mainda ameandika: "@shakoor jongo nakueshimu sana tena sana.ila kwa kuwa umeandika Habari kwa faida yako mwenyewe Mungu akubariki ila nasema hivi hakuna mtu atakae weza kunichafua ktk huu ulimwengu.1umeandika Habari yenye uongo mwanzo mwisho kwa mfano nikienda kukufungulia mashitaka utaniona mbaya Alafu mnazitaja hosptal za watu hamuoni kama mnazichafulia majina.sasa nikienda Hapo kwa mvungi wewe ndio ulionipeleka na hiyo Mimba itakuwa wewe ndio ulionipa.... acheni utoto alafu kitu kingine sijaongea na gazeti lolote sasa unaposema umeongea na mimi wapi kwa nini mnapenda kubuni mambo. plz plz sipendi mnapoandika upuuzi mkanichanganya na majina ambayo sihusiani nayo.kila mtu anamaisha yake hivyo sipendi kuchanganywa kwenye upumbavu.alafu unasema ulikuja kwangu ukaambiwa sipo labada nilikuwa kwako kama nilikuwa sipo.tusipende kukwazana ktk maisha.kiukweli kwa hili umenikwaza sana. Mungu wangu anaujua ukweli ataunichafue kwa njia zozote sichafuki.kwa taharifa tu ya haraka haraka mi siyo mzinzi kwa sasa huko nilishapita kitambo eeeeeeeh alafu Mimba ni jambo la heli siyo ukimwi huo useme niufiche. Nitazaa ndani ya Ndoa na si Nje ya ndoa. maana hata mimi nimezaliwa ndani ya ndoa why me nizae Nje ya ndoa hahahahaha me siyo kuku wala mnyama nijizalie ovyooooo.alafu umeandika nimetoa Mimba labda wewe ndio Ulikuwa Dk wangu ulinifanyia hilo tukio.....Mungu akubariki kwa Habari yako ila hili Gazeti watu watalisoma Leo kesho wamesahau na maisha yataendelea.Maana wiki iliyopita mliniandika nikaa kaa kimya sasa naona story mnaifanya endekevu kama tamthilia ya Isidingo vile."
uwiiiii Leo naona mmeamka na mimi nyinyi magazeti hivi naomba kuuliza Bado tu mkiandika habari za Ray na mimi mnaniweka kiruuuuuu mbona mimi nimesha sahau ata kama nilisha kuwana mahusihano na huyo mtu......jamani Ebu acheni maisha ya endeleeeeeeee me huko sipo tena alafu huwa sipendi mkiandika Habari zake nikawekwa sura yangu au jina langu coz me sihusiki ktk mambo yake na mimi siyo mzazi wa hao watu useme wakiandikwa kwenye magazeti me ni Ubini wao kwamba majina yao yakiandikwa langu lisipokuepo jina halijakamilika. Mbona hamtaki kuukubali ukweli. ni hivi Fungeni ukurasa wa Habari za huyo kaka na wanawake zake me kuniweka.me sihusiki na nilishalizungumzia hilo toka mwaka jana lakini naona mkitakakunogesha habari zenu za uongo mpaka muweke jina langu...Hahahahahahhahaha mnajua mnanichekesha sana. msinitafutia uadui na watu wapendwa coz me sitaki kujenga uadui na watu basi msinilazimieshe. Natamka Tena mimi na Ray we are over toka mwaka jana.so acheni hayo mambo ya kuniandika nae.andikene mambo yake na maisha yake na watu wake siyo uungwana kuniandika kunichanganya na mimi.@Gazeti la Kiu.