Refa Andre Marriner huenda akawekwa kando kwenye michezo ya mwishoni mwa juma baada ya kufanya makosa ya kutoa kadi nyekundu kwa mchezaji wa kwenye mchezo wa ligi kuu kati ya Arsenal na Chelsea ambapo Chelsea ilishinda 6 bila.
Marriner alitoa Penalti wakati wa mchezo wa siku ya Jumamosi baada ya Alex Oxlade-Chamberlain kushika mpira, lakini Kieran Gibbs alipewa kadi nyekundu na kuondolewa kimakosa.
Oxlade-Chamberlain alionekana akimwambia Refa kuwa yeye ndiye aliyeshika mpira, hata hivyo uamuzi wa awali ndio ulikua wa mwisho.
Hata hivyo baadaye Mariner alikiri na kuomba radhi kwa makosa yaliyojitokeza, akikiri kufanya makosa kutomtambua aliyepaswa kuadhibiwa katika mchezo huo.
Chama cha waamuzi wa mchezo wa kulipwa kimesema kuwa matukio ya kumwadhibu mchezaji kimamkosa ni nadra kutokea na mara nyingi husababishwa na sababu mbalimbali za kiufundi
SOURCE:BBC