Watu milioni saba walifariki mwaka
2012 kutokana na hewa chafu. Hii ni
kwa mujibu wa shirika la afya
duniani .
Ripoti ya shirika hilo inasema kuwa
kuna uhusiano mkubwa kati ya hewa
chafu na maradhi ya moyo, tatizo la
kupumua na ugonjwa wa Saratani.
Kifo kimoja kati ya vinane duniani
kilitokana na hewa chafu , na kuifanya
hali hiyo kuwa moja ya hatari ya
mazingira chafu afya ya binadamu.
Tarkriban watu milioni sita waliofariki
dunia walikuwa Asia ya Mashariki na
katika eneo la Pacific.
Shirika hilo limesema kuwa takriban
watu milioni 3.3 walifariki kutokana na
hewa chafu katika nyumba zao kwa
kutumia mkaa kukipikia na wengine
milioni 2.6 walifariki kutokana na
hewa chafu nje ya nyumba zao , hasa
katika nchi zinazostawi.
Afisaa mmoja mkuu wa shirika hilo,
Daktari Maria Neira, amesema kuwa,
hewa chafu ina hatari kubwa kwa afya
ya watu kuliko ilivyodhaniwa hasa kwa
kusababisha maradhi ya Moyo na
Kiharusi.
Ripoti hii inaonyesha umuhimu wa
kushirikiana katika kuhakikisha kuwepo
kwa hewa safi.
Shirika hilo limesema kuwa
kupunguzwa kwa viwango vya hewa
chafu kunaweza kuokoa maisha ya
watu.
Kadhalika shirika hilo limesema: "usafi
wa hewa tunayopumua unazuia
maradhi ya kuambukizana na pia
kuondoa hatari kwa watoto, wazee na
wanawake.''
Source:-bbc swahili.
2012 kutokana na hewa chafu. Hii ni
kwa mujibu wa shirika la afya
duniani .
Ripoti ya shirika hilo inasema kuwa
kuna uhusiano mkubwa kati ya hewa
chafu na maradhi ya moyo, tatizo la
kupumua na ugonjwa wa Saratani.
Kifo kimoja kati ya vinane duniani
kilitokana na hewa chafu , na kuifanya
hali hiyo kuwa moja ya hatari ya
mazingira chafu afya ya binadamu.
Tarkriban watu milioni sita waliofariki
dunia walikuwa Asia ya Mashariki na
katika eneo la Pacific.
Shirika hilo limesema kuwa takriban
watu milioni 3.3 walifariki kutokana na
hewa chafu katika nyumba zao kwa
kutumia mkaa kukipikia na wengine
milioni 2.6 walifariki kutokana na
hewa chafu nje ya nyumba zao , hasa
katika nchi zinazostawi.
Afisaa mmoja mkuu wa shirika hilo,
Daktari Maria Neira, amesema kuwa,
hewa chafu ina hatari kubwa kwa afya
ya watu kuliko ilivyodhaniwa hasa kwa
kusababisha maradhi ya Moyo na
Kiharusi.
Ripoti hii inaonyesha umuhimu wa
kushirikiana katika kuhakikisha kuwepo
kwa hewa safi.
Shirika hilo limesema kuwa
kupunguzwa kwa viwango vya hewa
chafu kunaweza kuokoa maisha ya
watu.
Kadhalika shirika hilo limesema: "usafi
wa hewa tunayopumua unazuia
maradhi ya kuambukizana na pia
kuondoa hatari kwa watoto, wazee na
wanawake.''
Source:-bbc swahili.