Ebwana nchi za Iran na Iraq zimeongoza katika kutekeleza adhabu zilizokithiri duniani ambapo mwaka jana asilimia 66 ya adhabu za kunyongwa zilitekelezwa kwenye hizi nchi.
Japo kuwa nchi chache sana zinatumia adhabu ya kifo duniani ukilinganisha na miaka 20 iliyopita, kuua wahalifu Iraq na Iran kumesaidia kuongezeka kwa asilimia 15 za adhabu za mauaji duniani, hii ni kutokana na utafiti wa Amnesty International kuhusu hukumu ya kifo.
Kuna watu 778 ambao wameuliwa kutokana na adhabu ya kifo duniania kwa mwaka 2013 pekee ambapo kwenye hiyo idadi, 538 ni ya Iran na Iraq pekee, ambapo rekodi ya dunia nzima kwa mwaka 2012 ilikua 682.
Amnesty international inasema mauaji ya uhalifu waliyoona katika nchi kama Iraq na Iran yalikuwa ni ya aibu.
Juzi kuna taarifa ilitolewa na wizara ya mambo ya nje ya Tanzania kuhusu idadi ya Watanzania waliofungwa kwenye magereza China wengine waliohukumiwa kunyongwa.
Sasa basi, kwenye hii taarifa ya leo iliyotolewa na shirika la Amnesty Internationa, hawahawa China wanaowashikilia Watanzania, wanaaminika kutoa adhabu hiyo kwa maelfu ya watu kwenye hizi rekodi, ikiwa ni zaidi ya hesabu ya dunia nzima lakini hakuna takwimu halisi juu ya hilo kutokana na mamlaka yao Beijing kusema takwimu hizo ni siri ya taifa.
Kwa Iran, Orodha iliyotoka 2013 ni ya mpaka watu 369, ambayo imeongezeka watu 55 kutoka 2012, lakini habari ni kwamba, mamia ya watu wengine wamepewa adhabu hiyo kisiri ambapo namba ya mauaji hayo katika Iran na Iraq karibu na 700.
Iraq wametoa adhabu kwa watu mpaka 169 ongezeko ya nusu na robo kutoka mwaka 2012, Saudi Arabia imetoa adhabu hiyo kwa watu 79 na Marekani ni watu 39 tu.
Kwa upande wa Africa, Benin, Ghana na Sierra Leone wamechukua hatua za kuanza kusitisha adhabu hii, Somalia imezidisha adhabu hii ambapo wameuwa watu 34 mwaka 2013 kutokana na adhabu ya kifo, na 6 tu mwaka 2012.
Na kwa marekani bado inaendelea kutumia adhabu hizo ambapo wengi walioadhibiwa wanatoka Texas.
Korea Kaskazini pia haina orodha kamili lakini inasemekana kuua watu wenye makosa ya dawa za kulevya, uasherati, kufuru na uenezaji wa picha za ngono na pia wamekua wakiua watu kwa makosa ya kuangalia video zisizoruhsiwa (banned videos) zinazotoka nchi jirani ya Korea Kusini.
Ripoti hii inasema zaidi ya watu 23,000 walikuwa katika orodha ya kuuwwa kwa adhabu ya kifo mwaka 2013 na watu 2,000 walikuwa wameshapewa hukumu ya kifo katika nchi 57 mwaka 2013.