Costa, mwenye umri wa miaka 25, amekuwa na rekodi nzuri ya kufunga mabao Hispania na amesaidia Atletico kutinga Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, ambako itamenyana na Barcelona.
Hadi sasa nyota huyo wa kibrazil mwenye uraia wa Hispania Katika La Liga amefunga mabao 23 katika mechi 28, wakati Ligi ya Mabingwa amefunga mabao saba katika mechi tano- na kufanya jumla ya mabao 30 aliyofunga hadi sasa katika mechi 33.