BAADHI YA BIDHAA ZITOLEWAZO NA PSI TANZANIA
Na Shija Felician
Kijukuu Blog Kahama.
WAFANYABISHARA wilayani Kahama wametakiwa kuzitumia bidhaa zitolewazo na Shirika lisilo la Kiserikali la Population Services International – PSI kwa lengo la kuikoa jamii dhidi ya maambukizi ya ugonjwa wa Ukimwi.
Hayo yameelezwa leo na Meneja Mawasiliano wa Shirika hilo la Kimataifa la PSI;Clement Mbogo wakati wa mahojiano maalumu na Mwandishi wa Kijukuu Blog yaliyofanyika mjini Kahama.
Katika mahojiano hayo bwana Mbogo amesema pamoja na kuwepo changamoto juu ya usambazaji wa bidhaa hizo ambazo ni Kondomu za kike na kiume,lakini Shirika linawapongeza kwa kazi wanayoifanya.
Amesema hivi sasa idadi kubwa ya wananchi wanajua matumizi ya kondomu kutokana na wafanyabiashara hao kuzisambaza zaidi bidhaa hizo ikiwa ni pamoja na dawa ya kutibu maji ambayo sasa jamii inajua umuhimu wa kutumia maji salama.
Pamoja na hali hiyo Shirika hilo lilikutana na viongozi mbalimbali wa serikali pamoja na wa Halmashauri ya Mji wakiwemo Wafanyabiashara ili kuwapongeza kwa usimamizi mzuri na hamasa waliyoitoa kwa wananchi juu ya matumizi hayo ya kondomu na maji salama.