- Ridhiwani ahakikishiwa kura kata ya Mandela
- Wananchi wa Chalinze wasema dhihaka zinazotolewa na wapinzani kuisha tarehe 6
- Wafugaji wamuunga mkono.
- Wapinzani warudisha kadi kama mvua
Mgombea Ubunge Jimbo la Chalinze kupitia CCM Ndugu Ridhiwani Kikwete akiomba kura kwa wananchi wa kijiji cha Kilemera kata ya Mandera. Mzee Robert Jerome mwenye umri wa miaka 92 ambaye ni Mwenyekiti Mstaafu wa Kijiji cha Kilemera akiongea na mgombea wa nafasi ya Ubunge kupitia CCM Ndugu Ridhiwani Kikwete Wananchi wa Kijiji cha Hondogo wakiitika kwa wingi wakati wa mkutano wa kampeni za Ubunge kupitia CCM uliofanyika kijijini hapo. Hussein Yahya akirudisha kadi yake ya Chadema kwa mgombea wa Ubunge wa CCM Jimbo la Chalinze Ndugu Ridhiwani Kikwete wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika kijiji cha Hondogo kata ya Mandera. Mbunge wa Kisarawe Ndugu Suleiman Said Jaffo akihutubia wananchi wa kijiji cha Kibaoni kata ya Mandera wakati wa mkutano wa kumnadi mgombea wa ubunge jimbo la Chalinze Ndugu Ridhiwani Kikwete. Ridhiwani Kikwete akiruka kimasai . Wakina mama wa kimasai wakifurahia ujio wa Ridhiwani Kikwete katika kijiji chao cha Umasaini Chatanga kitongoji cha Nameloki. Mmoja ya nyumba ya wafugaji wa kimasai wa kijiji cha Umasaini Chatanga kata ya Nameloki. Watoto wa wafugaji wa Kimasai wakiupungia mkono msafara wa mgombea ubunge kupitia CCM Ndugu Ridhiwani Kikwete. Kikundi cha Ngoma cha Mwamko wakicheza ngoma ya Selo ya kabila la wazigua wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika kijiji cha Makole ambapo Ridhiwani Kikwete alihutubia wakazi wa kijiji hicho kata ya Mandera. Mgombea Ubunge Jimbo la Chalinze kupitia CCM akiinua kadi za Chadema zilizorudishwa na vijana wa kijiji cha Makole kata ya Mandera wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika kijijini hapo.
Mgombea wa Ubunge kupitia CCM Ndugu Ridhiwani Kikwete ,Mbunge wa Simanjiro Ndugu Christopher Ole Sendeka wakiwa kwenye picha ya pamoja na kikundi cha ngoma cha Mwamko cha kijiji cha Makole.