Quantcast
Channel: Blogu ya Wananchi
Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

KINANA KUTUA SUMBAWANGA LEO KWA AJILI YA ZIARA YA MKOA WA RUKWA

$
0
0



Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana (Pichani), anatarajiwa kutua mjini Sumbawanga, leo saa tano asubuhi kwa ajili ya kuanza ziara ya kikazi mkoani Rukwa.

  Taarifa zilizopatikana kutoka Ofisi ya CCM mkoa wa Rukwa zilizopo mjini Sumbawanga zimesema, baada ya kuwasili Kinana atakwenda katika Ofisi ya CCM ya mkoa ambako atapewa taarifa ya Chama ya utekelezaji wa Ilani mkoani Rukwa na baadaye kufuatiwa na taarifa ya serikali kuhusu utekelezaji wa ilani hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, baada ya kupata taarifa za Chama na Serikali kuhusu utekelezaji wa ilani ya CCM, Kinana anaondoka mjini Sumbawanga na kwenda Wilaya ya Nkasi ambako ataanza rasmi ziara yake kwa kufanya mambo mbalimbali ikiwemo mikutano ya hadhara.
CCM Blog, Sumbawanga

Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>