INAUMA sana! Watoto wawili wa kiume wa familia moja, Daniel Paul (8) na mdogo wake, Emmanuel Paul (3), wamepoteza maisha wakiwa pamoja baada ya kuteketea kwa moto ndani ya nyumba.
Katika tukio lililojiri majira ya saa 1:00 asubuhi, maeneo ya Mtaa wa Rufita, Mwanza-Road mjini hapa baada ya nyumba waliyokuwa wakiishi kuteketea kwa moto huku wakiwa wamelala ndani.
Kamanda wa Polisi Wilaya ya Tabora, OCD, Samwel Mwampashe alithitisha kutokea kwa tukio hilo huku akiahidi kuwa polisi watafanya uchunguzi ili kubaini chanzo kamili cha moto huo.