- Juzi kulikuwa na habari kutoka Marekani kwamba kuna Mtanzania mwenzetu huko ambaye ameishi huko Miaka zaidi ya 30 amefariki Dunia, ndugu zake hawajulikani walipo na ni kina nani na kwamba mwili wake ulikuwa unakaribia kuchomwa na kutupwa baharini na serikali ya mji huko kwa kukosekana Dola Za Kimarekani USD $ 6,000 tu ambazo ni sawa kama Shillingi Millioni 10 za hapa home.

- Now kwanza kwa nini hakuwa na mawasiliano ya aina yoyote na ndugu zake huku home muda wote huo alipokuwa huko? Halafu miaka yote hiyo kwa nini hakuwa na Life Insurance? Na kwa nini hakuwa na mahusiano ya karibu na Wabongo wenziwe?

- I mean inaleta maswali mengi makubwa kuliko majibu, Miaka 30 USA kweli mtu unafikia mahali unakufa huna Dola $ 6,000 tu benki jamani? This is a shame na ninasema hivi kwa sababu najua sana kwamba kuna wengi mko huko kama huyu marehemu, badilikeni bwana mpo Ulaya huko Dunia ya kwanza fanyeni mambo japo kidogo kama Wazungu, haiwezekani ukaishi miaka yote hiyo huko ukakosa Life Insurance no way, sasa inaaanza kuwa kazi ya kuchangishana kwenye mitandao, na wala ndugu zako hawajulikani wapo wapi na ni kina nani? Please jamani hebu igeni japo kidogo mambo ya wazungu mimi pia nimeishi huko na mpaka leo bado ninayo my life insurance na pia nasubiri muda ufike niazne kukusanya mapesa yangu ya Retirement kwa sababu nililifanyia kazi Shirika moja kwa miaka 25, soon nitaanza kupumzika na malipo ya jasho langu la kuendesha Malori usiku na mchana haya ndio mambo unatakuwa kuyahangaikia ukiwa huko Ulaya jamani, hebu elimishaneni kidogo mbadilike kidogo tuondokane na hii aibu,

- I mean huku bongo kila unapopita unaanza kuulizwa maswali wewe eti wale wenzako vipi hawana Dola elfu sita tu miaka yote huko, badilikeni people wacheni mambo ya kizamani, kata life insuarnce na nunua kaburi mapema maana yanauzwa huko!!

Le Mutuz