Katika hali isiyokuwa ya kawaida na kushtua msanii mkongwe kiwanda cha Bongo movie nchini Miliamu Jolwa maarufu kama Jini Kabula ameibuka na kusema kuwa hakika gonjwa hatari la ukimwei litawateketeza wasanii wote wa Bongo movie na hakuna atakaebaki kama hawatobadilika kitabia.
Akiongea Sio siri kwa mfano leo hii wasanii wote bongo movie waseme wakamatwe kinguvu wakapimwe HIV utaona hali ilivyokuwa mbaya na sijui hata mmoja atakuwa mzima na sababu kubwa ni njaa ambapo sisi wengi wetu tuna majina lakini hatuna kitu hivyo hiyo hutoa nafasi ya kujirahisha ili kupata pesa" Alisem Kabula kwa uchungu.