Msanii nyota kwenye filamu za kibongo tu, Jackline Wolper ameibuka na kusema kuwa anachukizwa na wanafunzi wengi kujiingiza kwenye mapenzi wakiwa kwenye umri mdogo jambo ambalo nji hatari sana kwa future zao.
Akizungumza na Maskani Bongo msanii huyo alisema" Unajua sisi wakati tunasoma hatukuanza mapenzi mapema kama hawa watoto kiukweli mimi nimeanza kujua tendo nikiwa mtu mzima kabisa kwani nilikuwa naogopa sana lakini kwa sasa watoto hawa uwoga hata kidogo utakuta mwanamuziki ana miaka 12 ameshajua mapenzi hii ni hatari sana na akifisha miaka 18 si ndoa atakuwa balaa" Alisema Wolper kwa uchungu