Na Damas Makangale,
Mwanamke mmoja nchini Czech Republic ametolewa mawe takribani sita katika tumbo lake baada ya kufanyiwa oparesheni kubwa ya upasuaji na madaktari bingwa.
Madaktari wanasema alikuwa na hofu kubwa ya kuona madaktari kwa sababu ni nusu kifo ilikuwa ni kufa au kupona.
Alikaa na tumbo hilo kwa miaka 47 na lilikuwa likizidi kuvimba siku hadi siku ni mara 20 la tumbo la kawaida.
Wataalamu wanasema kwamba haijulikani kama atapata nafuu ya haraka na moja kwa moja ila baada ya oparesheni uzito wake ulipungua kwa kasi.
Mwanamke huyo raia wa Czesh alikuwa na takribani mawe sita ambayo yalioonekana na kutolewa kutoka kwenye tumbo lake na ukubwa wa tumbo ulikuwa mara ishirini la tumbo la kawaida.
Mwanamke huyo alifanyiwa oparesheni ya kuokoa maisha yake katika hospitali ya mkoa wa Zlin mwezi uliopita.
Ilichukua upasuaji wa zaidi ya saa saba kuondoa ukuaji ambao ni zaidi ya mita moja katika mduara wa kipimo cha kawaida.
Zdenek Adamik , mkuu wa Idara ya masuala ya uzazi na magonjwa ya wanawake katika hospitali hiyo, alisema madaktari walikuwa walishangazwa kwa nini mwanamke huyo akutafuta msaada wa matibabu mapema.
“Ni ajabu kwamba familia na marafiki wa karibu hawakuweza kupeleka taarifa katika mamlaka za utabibu mapema au kuguswa na matatizo ya mama huyo,” alisema mkuu huyo wa idara.
Chupa za Damu zilizotumika kumwogezea Damu mama huyo wakati wa Oparesheni iliyodumu masaa saba.