Stori: Gladness Mallya na Hamida Hassan
MAMA wa msanii wa filamu za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ ametupiwa tuhuma nzito kuwa ni mnywaji wa pombe sana hali inayomfanya mwanaye huyo alalamikie pembeni.
MAMA wa msanii wa filamu za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ ametupiwa tuhuma nzito kuwa ni mnywaji wa pombe sana hali inayomfanya mwanaye huyo alalamikie pembeni.
![](http://api.ning.com/files/79FAz6LP6HgK6oFOvz6gbeVmw3Lh4EAcyCYFC8f81LOsXTOGr-IhWwDkzrbQ6UGJqJwTg8HKcqVwqYie9-g186uhW8tKcShJ/MamaLulu.jpg?width=650)
Chanzo kliliendelea kutiririka kuwa, kutokana na Lulu kuchoshwa na tabia ya mama yake kutaka fedha na kila jioni kwenda baa, aliamua kumnunulia bodaboda ambayo inamuingizia fedha ambazo inadaiwa pia, kila akizipata huenda baa kulewa.
“Mama Lulu analewa mpaka sana, halafu anamlalamikia mwanaye kwamba ni mgumu hali ambayo inamuweka Lulu njiapanda,” kilisema chanzo hicho.
Baada ya kupata habari hizo paparazi wetu alimtafuta Lulu, ikasemekana yupo safarini na hakuwa hewani. Mapaparazi wetu walimtafuta mama yake na kumsomea madai yanayoelekezwa kwake, cha ajabu aling’aka na kusema:
“Sijanunuliwa bodaboda na Lulu yeye ndiye kasema ameninunulia au? Kwanza simtegemei Lulu mbona alipokuwa gerezani nilikuwa ninaishi vizuri tu namlea mwanangu na mama yangu, iweje leo nishindwe?
![](http://api.ning.com/files/79FAz6LP6HjLyh2iG3q19-OA5r3AgSyFjkyyl6F-b14M43oG94tLmlCuwG9SEtn7I-K6rZECP0OhmDIv*9xmEQMScbJ4ayXv/BGI6Q56CUAEdAyZ.jpglarge.jpg?width=650)
Mara kadhaa vyanzo tofauti vimekuwa vikipenyeza habari Global kwamba mama huyo amekuwa akionekana katika ‘viwanja’ tofauti vya kula raha, ikidaiwa kuwa ni mtumiaji mzuri wa ‘mambo yale’.
-GPL