Wimbo mpya wa mfalme wa wa Pop, marehemu Michael Jackson uliopewa jina la ‘Do You Know Where Your Children Are? Ambao utatoka May mwaka huu umedaiwa kubeba ujumbe mzito kwa wazazi.
Kwa mujibu wa ripoti zinazodaiwa kutolewa na Epic Records, wimbo huo unazungumzia simulizi la mtoto wa miaka 12 ambaye alikuwa akiishi na baba yake wa kambo aliyemnyanyasa na hivyo kuamua kukimbilia mitaani ambapo aliishia kuwa kahaba.
“She wrote that she is tired of step-daddy using her/Saying that he'll buy her things, while sexually abusing her.” Aliandika Michael Jackson kwenye wimbo huo.
Mwenyekiti wa Epic Recods ameeleza nia ya kuuachia wimbo huo, “we are extremely proud and honoured to present this music to the world.”
Wimbo huo utakuwa miongoni mwa nyimbo 8 mpya ambazo zinatarajiwa kutoka zikiwa chini ya Epic Records na inaaminika kuwa Michael aliandika wimbo huo baada ya kukutwa hana hatia katika kesi ya unyanyasaji kijinsia wa watoto wa kiume mwaka 2005.