YANGA SC imekata rufaa dhidi ya mchezaji Mohammed Neto wa Mgambo Shooting ikidai anacheza Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kinyume cha kanuni za usajili. Yanga SC wanalalamikia usajili wa mchezaji huyo una mapungufu kwa kuwa ni raia wa kigeni, lakini hana Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC).
Ubingwa mezani? Kikosi cha Yanga iliyokata rufaa kutaka kukombo pointi ilizopoteza kwa Mgambo |
Mohamed Neto wa Mgambo JKT akichuana na William Lucian 'Gallas' wa Simba katika Ligi Kuu msimu huu mechi ya mzunguko wa kwanza.Mchezaji huyo amekatiwa rufaa na Yanga |