Quantcast
Channel: Blogu ya Wananchi
Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

LE MAJANGAZ & BONGO:- CHUNGU CHA AJABU KILIPONASWA JUU YA KABURI LA WATU KIKIFUKA MOSHI LIVE!!

$
0
0

MAUZA uza matupu kaburi la mtoto Agnes Mlawa (8) mkazi wa Ilala katika Manispaa ya Iringa aliyezikwa mwaka jana na leo baba wa mtoto huyo kakuta chungu cha ajabu chenye damu,maini na kichwa cha ndege kimechimbiwa kaburini. Tukio hilo la aina yake limetokea leo majira ya saa 2 asubuhi katika makaburi ya Makanyagio mjini Iringa wakati baba mzazi wa mtoto huyo Bw. Mlawa wakati akichembua kaburi hilo na mara baada ya kumaliza ghafla alishuhudia tukio hilo la chungu cha ajabu kuibuga juu ya kaburi hilo . 
" mimi hapa leo nilikuja kusembua kaburi la mwanangu ila baada ya kumaliza ghafla nilikuta kama damu zinaruka juu kutoka kaburini na baada ya kuchunguza ndipo nilipoona chungu hicho kikiibuka huu ya kaburi " 
Alisema kuwa chungu hicho kilikuwa kimefungukwa na kitambaa cheusi juu ambacho kimelowa dawa na kufungwa kamba ya nguo ya kijani na kutokana na tukio hilo la ajabu alilazimika kuacha jembe juu ya kaburi na kukimbia kuita watu wanaopita barabarani ili kuomba msaada zaidi. 
Mzazi huyo anadai kuwa mazingira ya kifo cha mtoto wake yalikuwa ni ya kushangaza baada ya kuugua kwa muda wa siku nne pekee na kufariki dunia . 
Hata hivyo alisema kwa kuwa kwa upande wake haamini mambo ya kishirikiana hakuona sababu ya kumwita mganga wa kienyeji kwa ajili ya kushughulikia kuchoma chungu hicho na badala yake kuamua kuifanya kazi hiyo mwenyewe hasa akiamini nguvu ya Mungu zaidi.

" Napenda kuwashukuru wananchi waliofika hapa kwa kunitia nguvu na pia kuwashukuru madereva boda boda akiwemo kijana Ahmed kwa kujitolea mafuta ya Petrol kwa ajili ya kukichoma chungu hiki "

Mbali ya mzazi huyo kujitolea kuchuma chungu hicho na kuteketeza vitu vilivyo kuwemo ndani wananchi waliofika kushuhudia tukio hilo walilazimika kutimua mbio kuhofu zoezi hilo la uchomaji wa tunguli hizo.
Chungu cha ajabu kilichokutwa juu ya kaburi katika makaburi ya Makanyagio mjini Iringa leo kikiwa kinafoka damu
Wananchi wakishuhudia chungu hicho cha ajabu kushoto karibu na jembe
Hapa ndipo chungu hicho kilipoibukia
Baba wa mtoto Agnes Mlawa akichimbua chungu hicho
baba wa mtoto huyo kulia akisaidiwa na msamalia mwema kufungua chungu hicho ili kuona ndani
Hivi ndivyo vilivyokuwemo ndani na damu ,maini na kichwa cha ndege
Hapa msamaria mwema akionyesha vitu vilivyopo ndani
Mzee Mlawa akiwasha kiberiti kwa ajili ya kuteketeza ushirikiana huo
Tunguli ikiteketezwa kwa moto
Wananchi na mzee Mlawa kulia wakitazama tunguli hilo likiteketea kwa moto
Mwisho wa ushirikina hapa
MAUZA uza matupu kaburi la mtoto Agnes Mlawa (8) mkazi wa Ilala katika Manispaa ya Iringa aliyezikwa mwaka jana na leo baba wa mtoto huyo kakuta chungu cha ajabu chenye damu,maini na kichwa cha ndege kimechimbiwa kaburini.

Tukio hilo la aina yake limetokea leo majira ya saa 2 asubuhi katika makaburi ya Makanyagio mjini Iringa wakati baba mzazi wa mtoto huyo Bw. Mlawa wakati akichembua kaburi hilo na mara baada ya kumaliza ghafla alishuhudia tukio hilo la chungu cha ajabu kuibuga juu ya kaburi hilo .

" mimi hapa leo nilikuja kusembua kaburi la mwanangu ila baada ya kumaliza ghafla nilikuta kama damu zinaruka juu kutoka kaburini na baada ya kuchunguza ndipo nilipoona chungu hicho kikiibuka huu ya kaburi "

Alisema kuwa chungu hicho kilikuwa kimefungukwa na kitambaa cheusi juu ambacho kimelowa dawa na kufungwa kamba ya nguo ya kijani na kutokana na tukio hilo la ajabu alilazimika kuacha jembe juu ya kaburi na kukimbia kuita watu wanaopita barabarani ili kuomba msaada zaidi.

Mzazi huyo anadai kuwa mazingira ya kifo cha mtoto wake yalikuwa ni ya kushangaza baada ya kuugua kwa muda wa siku nne pekee na kufariki dunia .

Hata hivyo alisema kwa kuwa kwa upande wake haamini mambo ya kishirikiana hakuona sababu ya kumwita mganga wa kienyeji kwa ajili ya kushughulikia kuchoma chungu hicho na badala yake kuamua kuifanya kazi hiyo mwenyewe hasa akiamini nguvu ya Mungu zaidi.

" Napenda kuwashukuru wananchi waliofika hapa kwa kunitia nguvu na pia kuwashukuru madereva boda boda akiwemo kijana Ahmed kwa kujitolea mafuta ya Petrol kwa ajili ya kukichoma chungu hiki " Mbali ya mzazi huyo kujitolea kuchuma chungu hicho na kuteketeza vitu vilivyo kuwemo ndani wananchi waliofika kushuhudia tukio hilo walilazimika kutimua mbio kuhofu zoezi hilo la uchomaji wa tunguli hizo.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

Trending Articles

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>