LILE gari aina ya BMW X6 alilokuwa akitanulia mwigizaji Jacqueline Wolper linaendelea kuoza katika yadi ya Majembe, Mwenge jijini Dar kutokana na kudaiwa ushuru.
Taarifa ambazo Risasi Jumamosi limezipata kutoka katika vyanzo tofauti, zimeeleza kuwa hakuna uwezekano wa gari hilo kurudi katika mikono ya Wolper kwani aliingizwa mkenge tangu aliponunuliwa na aliyekuwa mpenzi wake, Abdallah Mtoro ‘Dallas’.
“Wolper aliingizwa mkenge tangu aliponunuliwa lile gari, lilikuwa linadaiwa ushuru sasa yeye bila kujua akaingizwa mkenge na pedeshee Ndama na kisha mtego wa kulinasa ukafanyika, Ndama huyohuyo akaja kumgeuka akawa anaeneza uvumi kuwa Wolper kaingizwa mkenge,” kilidai chanzo.
Akizungumza na paparazi wetu hivi karibuni, Wolper aliweka bayana kuwa gari lile alilonunuliwa kwa dola 130,000 (zaidi ya Sh. Mil. 170 ) kipindi penzi lake na Dallas lilipokuwa likichanua, mwaka jana polisi wa kimataifa (Interpol) kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) walilikamata kwa kudaiwa ushuru.
“Sina ujanja tena kwani hata mimi nilikuwa sijaelewa kama linadaiwa lakini Ndama ndiye aliyejua mchongo mzima, akaniingiza chaka. Hadi sasa linaozea pale Majembe, sina jinsi, namuachia Mungu,” alisema Wolper na kuongeza:
“Nilipolikabidhi Majembe na kuonesha documents (nyaraka) zote, niliambiwa nitalipata baada ya muda lakini mpaka leo sijaambiwa lolote. Linaozea pale.”
Chanzo:Global P