Quantcast
Channel: Blogu ya Wananchi
Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

HUKUMU YA KESI YA KINA KIBANDA NA MAKUNGA SASA NI JANUARI ONA TAREHE!!

$
0
0


Meneja Uendelezaji Biashara wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL), Theophil Makunga.PICHA|MAKTABA 


Ni ile inayodaiwa kuruhusu kuchapishwa kwa makala ya uchochezi kwa vikosi vya ulinzi mwaka jana.

Dar es Salaam.Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, inatarajia kutoa hukumu ya kesi ya makala ya uchochezi inayomkabili Meneja Uendelezaji Biashara wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL), Theophil Makunga na wenzake wawili, Januari 29, mwaka huu.
Hakimu Mkazi, Waliarwande Lema, alisema jana kuwa atatoa huku hiyo baada ya upande wa mashtaka na utetezi kumaliza kutoa ushahidi wao.
Licha ya kutoa ushahidi, Lema alisema pande zote zilipewa fursa nyingine ya kuwasilisha majumuisho yao ya mwisho ili kuweka wazi kama washtakiwa hao wana hatia ama la.
Hatua hiyo ilitokana na upande wa mashtaka, kuiomba mahakama kutoa nafasi hiyo kwa pande zote mbili kuwasilisha majumuisho ya mwisho.
Upande wa utetezi ulikamilisha hatua hiyo kwa kuwasilisha majumuisho yao tangu mwishoni mwa wiki iliyopita.
Hata hivyo, upande wa mashtaka haukuwasilisha majumuisho na Hakimu Lema akasema kwa sasa pande zote zisubiri mahakama kutoa uamuzi wake.
Awali kesi hiyo ilianza kusikilizwa kwa upande wa mashtaka kuwaita mashahidi watatu, Mkurugenzi Msaidizi wa Usajili wa Magazeti, Raphael Hokororo, Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Magereza (ACP), George Mwambashi kutoka Kitengo cha Sheria cha kikosi hicho na Mrakibu Mwandamizi wa Jeshi la Polisi (SSP), David Hizza.
Baada ya washtakiwa hao kumaliza kutoa ushahidi wao, Wakili wa Serikali, Beatha Kitau alifunga ushahidi, mahakama ikaupitia na kuwaona washtakiwa wana kesi ya kujibu.
Makunga na wenzake, Absalom Kibanda na Samson Mwigamba wanakabiliwa na kesi ya uchochezi dhidi ya askari wa majeshi ya ulinzi kwa kuchapisha makala kwenye Gazeti la Tanzania Daima yenye maneno yaliyolenga kuwashawishi wasiwatii viongozi wao.
Makala hayo ya Novemba 30, 2012 inayodaiwa kuwa ni ya uchochezi ilikuwa na kichwa cha habari ‘Waraka maalumu kwa askari wote.’
Makala hayo yaliandikwa na Samson Mwigamba kupitia safu yake ya ‘Kalamu ya Mwigamba’ katika gazeti hilo. Washtakiwa hao wanatetewa na mawakili Nyaronyo Kicheere, John Mhozya, Frank Mwalongo na Mabere Nyaucho.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>