Masanii wa filamu, Kajala Masanja amedai kuumizwa na watu wanaojiita ‘Team Wema’ kwa kumzushia kuwa anatembea na mume wa zamani wa rafiki yake, Wema Sepetu na kudai kuwa anatarajia kumtafuta Wema ili kuzungumza naye.
“Mimi ningependa hawa Team Wewa ndio wangezungumza na ndio wameanzisha. Sina tatizo na Wema, kwahiyo hao ndio wanajua mimi sijui. Hata bwana wake huyo simjui,mimi aliyeanzisha simjui ila kama unakumbuka nilianza kuzushiwa ya mume wa Shamim leo wanasema mume wa Wema labda ndio vinawafurahisha. Yaani mimi sijui chochote,sijaonana na Wema. Wema alikuwa busy anashoot movie yake na mimi nilikuwa mimesafiri nimeenda kwa bibi yangu labda sasa hivi aliporudi ndipo nitamcheki tuzungumze,” amesema Kajala.
Credit: Bongo5