Miili mitatu (3) ya waliosemekana ni majambazi ikiteketea kwa moto mara baada ya kushindwa kufanya uvamizi katika kibanda cha tigo pesa maeneo ya Tabata Shelly.
Inasemekana raia waliokuwepo eneo hilo waliushitukia mchezo na kuweka mtego hadi kuwanasa vyema hayo majambazi, ilidaiwa kuwa majambazi mawili yalikuwa katika pikipiki na mmoja wao alitangulizwa kwa miguu na walipotaka kufanya uvamizi huu walijikuta hali si shwari kwao na kujinasisha mikononi mwa wananchi waliochukua uamuzi wa kuwachoma moto pamoja na pikipiki yao.