STAA wa sinema za Kibongo, Flora Mvungi amefunguka kuwa ubize wa kulea mwanaye ndiyo umemfanya avunje urafiki na shosti wake, Salma Jabu ‘Nisha’.
Flora alifunguka hayo juzikati baada ya paparazi wetu kumuuliza juu ya taarifa zinazodai kuwa wawili hao wamepishana kauli na kila mmoja kuishi kivyake.
“Sina tatizo kiivyo na Nisha lakini labda niseme tu mtoto ndiye amenifanya mimi na Nisha tuwe mbalimbali, hakuna kingine,” alisema Flora.