Mvua zinazoendelea kunyesha Mikoa tofauti Tanzania bado zimeendelea kuleta madhara licha ya taarifa ya Watanzania kadhaa kukosa makazi bado miundombinu inayounganisha Dar es salaam na mikoani imekua ni tatizo kubwa.
Daraja la Mto Mzinga ambao pia ndilo linalounganisha Dar na mikoa ya Kusini limebeguka kipande kufuatia mvua iliyonyesha na inayoendelea kunyesha,Wasafiri wa kwenda
Nachingwea,Masasi,Tunduru,Mtwara,Lindi na maeneo jirani wameendelea kupata shida ya usafiri.
Baadhi ya kampuni ambazo zinamiliki zaidi ya mabasi manne wamekua wakifaulisha wasafiri toka Basi ambalo limekwama upande wa Mtwara kuingia kwenye basi lililo upande wa Dar na wa Dar kuingia basi la Mtwara ili kufanya Safari ziendelee.
Miongoni mwa wasafiri ambao wamekwama kusafiri ni pamoja na Tundaman ambaye alikua na show leo Maisha Club Mtwara,hizi ni baadhi ya picha kwenye eneo lililokatika Daraja hilo.