Asubuhi April 13 2014 makamu wa Rais Dr. Mohammed Gharib Bilal, mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Said Mecky Sadick na Kamanda wa polisi kanda maalum ya Dsm Suleiman Kova walipata ajali ya Helikopta iliyoanguka uwanja wa ndege Dar wakitaka kutembelea sehemu zilizo athirika na mafuriko.
Mwandishi mmoja aliekuepo kwenye ndege hiyo aliongea kwa
ufupi anasema wakati wanaanza kupaa, ni kama upepo mkali ulikua unaivuta Helikopta kurudi nyuma ikiwa imepaa urefu wa kama futi tano ambapo ilizidiwa nguvu na kugonga paa kisha ikaanguka.
Baada ya ajali walijitazama wakaona ni wazima isipokua michubuko midogomidogo kisha wakarudi kwenye magari yao na kuyatumia kuelekea moja kwa moja kwenye maeneo waliyokua wamepanga kwenda kwa Helikopta.
Makamu wa Rais akionyeshwa na katibu mkuu wa wizara ya ujenzi Injinia Mussa Iombe, sehemu ya daraja la Mpiji linalounganisha Bagamoyo na Dar es Salaam lililokatika kutokana na mvua kubwa.
Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal akitoa maelekezo kwa katibu mkuu wa wizara ya Ujenzi Injinia Mussa Ibrahim Iombe wakati alipotembelea kukagua maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Mpiji lililokatika kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha, katikati ni mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Said Mecky Sadick.
Malori yakiendelea kumwaga vifusi vya mawe kwenye daraja hilo
Nguzo za umeme baada ya kuzidiwa nguvu na maji yaliyobomoa daraja.
Picha zote zimepigwa na OMR