Seth Bosco.
MSANII wa filamu ambaye ni mdogo wa marehemu Steven Kanumba, Seth Bosco amefunguka kuwa marehemu kaka yake huyo amemchanganya kimaisha kwani kila kukicha hajui atafanya nini kwa siku nzima. Seth alisema, tangu Kanumba afariki akiamka asubuhi hajui anafanya nini kwa siku nzima tofauti na alivyokuwa hai walikuwa wakipanga ratiba ya siku hata kama wamerudi nyumbani usiku wa manane lazima wapange ratiba ya siku inayofuata.“Siku hizi nikiamka sielewi nafanya kazi gani kwa siku nzima jambo ambalo linanifanya nimkumbuke sana Kanumba kwani alipokuwa hai tulikuwa tukipanga ratiba za siku inayofuata usiku tofauti na sasa,” alisema Seth.