Siku mbili zilizopita stori mbalimbali kwenye mitandao zilihusu msanii wa longtime kwenye bongofleva aitwae Dudubaya kudaiwa kumkata sikia Mama yake mkubwa kwa kinachosemekana kuwa tuhuma za kichawi lakini siku moja baadae Dudubaya alikanusha kupitia U Heard ya XXL Clouds FM kwamba hajamkata bibi yake sikio, yeye sio mtu wa kufanya hicho kitendo.
Sasa leo Mama mkubwa huyu wa Dudubaya amezungumza na Waandishi wa habari na kuthibitisha kweli kukatwa sikio na Dudubaya ambapo shahidi mwingine aliyezungumza ni mjukuu wake.
Maelezo waliyoyatoa ambayo ndio yamenifikia sasa hivi yatawekwa hapa baadae
Sehemu aliyokatwa imezibwa kwa makusudi.
Chanzo:millardayo.com