MUUZA sura wa sinema za Kibongo, Shamsa Ford amesema wasanii wengi wenye majina makubwa wamekuwa wakiringia umaarufu wao na kuwadharau wengine jambo ambalo halina manufaa zaidi ya kuwashushia heshima.
Akipiga stori na paparazi wetu, alisema kuna wasanii ambao ‘wametoka’ huwaonyesha dharau wenzao kwa kujivunia kujulikana kwao mbele ya jamii.
“Binafsi namthamini kila mtu, lakini utakuta mwingine hata unataka ufanye naye kazi, lakini kwa kujiona yeye ni staa zaidi basi hata muda mliopanga hatauzingatia akihisi utamnyenyekea, hiyo siyo maana ya ustaa watu wajitambue,” alisema bila kuwataja majina wahusika.
-GPL