KATIKA kuelekea sikuu za Krismasi na Mwaka mpya pilika pilika zimeongezeka katika mji wa Moshi na mkoa wa Kilimanjaro kwa ujumla huku vibaka pia wakiendelea na udokozi na wizi wa vitu mbalimbali.Katika kuthibitisha hilo juzi Tanzania Daima limeshuhudia mkazi wa kijiji cha Nshara, Machame wilayani Hai,ambaye jina lake halikupatikana mara moja amenusurika kuuawa kufuatia kipigo kutoka kwa wananchi wenye hasira kumshambulia kwa silaha za jadi baada ya kuiba kitoto cha nguruwe maarufu kama "Kiti moto".Tukio hilo la aina yake ambalo linaashiria maandalizi ya siku kuu hizo lilitokea juzi majira saa 5.30 asubuhi kijijini humo baada ya mkazi huyo kuonekana akiwa amembeba mnyamya huyo begani akiwa katika mfuko,maarufu kama Sandarusi mithili ya mzigo wa kawaida.Akizungumzia tukio hilo,mkazi wa kijiji cha Nshara, Husein Mbaruku alisema mtu huyo alionekana akinyata katika banda la Nguruwe akiwa na mfuko wake akiamini kuwa hakuna mtu aliyemuona ingawa wenyeji nao walikuwa wakimvizia ili kuona anachotaka kufanya.
KATIKA kuelekea sikuu za Krismasi na Mwaka mpya pilika pilika zimeongezeka katika mji wa Moshi na mkoa wa Kilimanjaro kwa ujumla huku vibaka pia wakiendelea na udokozi na wizi wa vitu mbalimbali.
Katika kuthibitisha hilo juzi Tanzania Daima limeshuhudia mkazi wa kijiji cha Nshara, Machame wilayani Hai,ambaye jina lake halikupatikana mara moja amenusurika kuuawa kufuatia kipigo kutoka kwa wananchi wenye hasira kumshambulia kwa silaha za jadi baada ya kuiba kitoto cha nguruwe maarufu kama "Kiti moto".
Tukio hilo la aina yake ambalo linaashiria maandalizi ya siku kuu hizo lilitokea juzi majira saa 5.30 asubuhi kijijini humo baada ya mkazi huyo kuonekana akiwa amembeba mnyamya huyo begani akiwa katika mfuko,maarufu kama Sandarusi mithili ya mzigo wa kawaida.
Akizungumzia tukio hilo,mkazi wa kijiji cha Nshara, Husein Mbaruku alisema mtu huyo alionekana akinyata katika banda la Nguruwe akiwa na mfuko wake akiamini kuwa hakuna mtu aliyemuona ingawa wenyeji nao walikuwa wakimvizia ili kuona anachotaka kufanya.