Mkongwe kwenye sanaa Bongo, Blandina Chagula ‘Johari’.
MKONGWE kwenye sanaa Bongo, Blandina Chagula ‘Johari’ amefunguka kuwa endapo ikitokea mkurugenzi mwenzake, Vincent Kigosi akaoa, yeye atajitolea kuwa mwandaaji wa chakula. Akizungumza na mwanahabari wetu mwishoni mwa wiki iliyopita, Johari alisema yeye na Ray ni watu wa karibu kwa kuwa wameiongoza kampuni yao kwa muda mrefu hivyo katika jambo muhimu kama la ndoa, lazima ajitoe kinaga ubaga kufanikisha.
“Yani hata kama ikitokea kesho mkasikia Ray anaoa ujue kabisa nitakuwa muaandaji kuhakikisha madikodiko yanawafikia waalikwa kwa wakati muafaka,” alisema Johari ambaye mara zote amekuwa akikanusha kuwa uhusiano wa kimapenzi na Ray.