Mfungaji wa mabao mawili ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars katika sare ya 2-2 na Uganda, The Cranes kwenye Robo Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge, Mrisho Ngassa akiwa ameketi benchi Uwanja wa Manispaa, Mombasa, Kenya baada ya kutoka dakika ya 80 alipoumizwa na wachezaji wa Uganda. Hata hivyo, Stars ilishinda kwa penalti 3-2 baada ya sare hiyo ya 2-2 ndani ya dakika 90. Picha zinazofuatia ni namna Ngassa alivyoumizwa kidevuni kwa kiwiko na kwanga la mguu lililomuumiza kifundo cha mguu. Na picha nyingine ni wakati anaumizwa uwanjani.